Saturday, 06 October 2012 20:19

Kuitwa Kwenye Usaili-Utumishi Featured

Rate this item
(0 votes)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Kumb. Na. EA.7/96/01/C/49 21 Septemba, 2012
KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatangazia waombaji wa fursa za ajira kwa tangazo lililotolewa tarehe 25/05/2012 kuwa wamechaguliwa kufanya usaili, hivyo waendelee kujiandaa. Usaili huo utahusisha kada zifuatazo Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la II , Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III, Afisa Mtendaji Mtaa II, Afisa Mtendaji Mtaa III, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, Mpishi Daraja la II, Afisa Utamaduni Msaidizi, Mtakwimu Msaidizi, Dereva Daraja la II, Mhudumu wa Jikoni/ Mess Daraja la II, Mlezi wa Mtoto Msaidizi, Operata wa Kompyuta Msaidizi, Msaidizi Misitu Daraja La II, Msaidizi wa Ofisi, Msaidizi Ustawi wa Jamii Daraja la II, Maendeleo ya Jamii Msaidizi Daraja la II, Mpokezi, Katibu Mahsusi Daraja la III na Mlinzi


Ratiba rasmi ya usaili itatolewa baadae ikionesha mahali, muda na tarehe ya kufanyika usaili husika.
Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. KUJA NA KITAMBULISHO KWA AJILI YA UTAMBUZI MFANO: KITAMBULISHO CHA MKAZI, KUPIGIA KURA, BENKI, KAZI, HATI YA KUSAFIRIA N.K
2. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) za kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.


3. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
4. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
5. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.


6. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
7. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
8. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Read 5453 times