Wednesday, 25 March 2015 00:00

13,000 uzaliwa na matatizo ya moyo

Dk Namala Mkopi,(PICHA/LM)

Na Mwandishi wetu

Inasemekana zaidi ya watoto 13,000 nchini Tanzania wanazaliwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo,ambapo alisilimia 25%imeelezwa kuwa wanahitaji matibabu mara baada ya kugundulika kuwa na matatizo hayo.

Aidha, kwa mujibu wa takwimu mwaka 2013/14 watoto 330 walikuwa na mahitaji ya matibabu huku idadi ya watoto 128 kati ya hao walipatiwa matibabu ya upasuaji

Taarifa hiyo ilitolewa na makamu wa rais wa chama cha madaktari wa watoto Tanzania Dk Namala Mkopi wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,ambapo pia amesema kuwa kwa kushirikiana na asasi ya Save children Heart ya nchi Israel na Hospitali ya Muhimbili(MNH) wameamua kuratibu mchakato huo kwa lengo la kutambua watoto wenye tatizo hilo na kuwapatia tiba ikiwamo upasuaji.

Alisema kuwa, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kuanzisha kitengo maalum cha kutoa huduma za kisasa, vipimo ambavyo vinaweza kugundua magonjwa ya moyo kwa watoto.“Pamoja na kitengo hiki kufanya baadhi ya matibabu bado hakijaweza kufanya upasuaji hususanI kwa watoto kutokana na hilo wizara ya afya inajitahidi kuwapeleka watoto hawa nchini India kwa ajili ya upasuaji,” alisema Dk. Mkopi.

Chama hicho kimeingia makubaliano na asasi hiyo, ili kuwasafirisha nchini Israel, watoto wenye ugonjwa wa moyo kupatiwa matibabu, vilevile watagharamiwa huduma zote.

Read 1761 times