Thursday, 26 February 2015 00:00

18 Mbaroni Vurugu za Iringa.

Kufuatia vurugu azilizojitokeza mkoani Iringa jana baina ya jeshi la polisi na wananchi katika eneo la mji wa Ilula kijiji cha Dinginayo wilayni kilolo  askari watano wamejeruhiwa na raia wawili huku mwananmke mmoja kaipoteza maisha.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani Iringa Pudensia Protas amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo zilizotokea majira ya sane asubuhi na tayari jeshi la polisi linawashikilia watu 18 kwa mahijiano na zaidi.

Vurugu hizo zilisababisha kifo cha mwananmke mmoja aliyejulikana kwa jina Mwanne Mtandi,pamoja na uharibifu wa mali za jeshilapolisi ikwemo gari,pikpiki na uvunjifu wa jengo la polisi kwa kuvunja vioo.

 Aidha kamanda amesema kuwa fujo hizo zilisababishwa na operesheni kuhusu uuzaji wa pombe za kienyeji na makosa mbalimbali kwa wananchi huku akiwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi ili kuepusha majanga kama hayo.

Hata hivyo katika vurugu hizo,wananchi wamegomea polisi mwili wa mwanamke huyo aliyefariki kutokana na vurugu hizo na kwa shinikizo la kuachiwa kwa watuhumiwa 18 waliokamatwa na jeshi la polisi.

 

Read 1845 times