Friday, 13 March 2015 00:00

40 WAAPISHWA UTUMISHI WA MAHAKAMA

Jaji Othmani Chande,(PICHA/LM)

Kufuatia kuwepo kwa mrundikano wa kesi zinazohusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi,kutokana na kukamatwa kwa watu wanaohusika kutotolewa huku kutokana na uchunguzi dhi yao,Idara ya Mahakama nchini imeahidi kukamilisha haraka kesi zote zinazohusu ukatili kwa watu wenye Ualbino pamoja na vikongwe.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam Jaji Mkuu wa TANZANIA Mohamed Othman Chande baada ya kushuhudia kuapishwa kwa Wasajili na Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani

Jaji Mkuu ameongeza kuwa idara ya Mahakama nchini inaendelea kuboresha huduma zake ili wananchi waweze kuhudumiwa kwa wakati.

Zaidi ya Wasajili na Naibu Wasajili Arobaini wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani wameapishwa wakati hafla hiyo baada ya kuteuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

 

 TBC

 

 

Read 1379 times