Friday, 06 February 2015 00:00

680milioni kutumika Ujenzi mradi wa maji Uvinza

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha KASHAGULU wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamesema kuwa kuanza kwa ujenzi wa skimu ya umwagailiaji kijijini hapo kunatoa matumaini kwa wananchi kuongeza kasi ya kuondokana na umaskini kupitia sekta ya kilimo

Wameutaja mradi huo utakapokamilika kuwa utawezesha wakulima kulima mazao ya Mpunga, Mahindi, Maharage na Mbogamboga mwaka mzima tena kwa utalaam zaidi tofauti na hapo awali kwani wanaimani kwamba watapatiwa elimu ya kilimo chenye tija zaidi.

Ujenzi huo wa mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha KASHAGULU ambao kwa awamu ya kwanza utahusisha hekta 500 kati ya 1000 ni miongoni ya mikakati ya Wilaya ya Uvinza ya kuogenza tija ya uzalishaji wa mazao yatokanayo na kilimo cha umwagiliaji.

Kwa mujibu wa afisa kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Uvinza Daniel Kamwela jumla ya shilingi milioni 680, zitatumika katika ujenzi wa mradi wa umwagiliaji hadi kukamilika kwake.

KAMWELA ameongeza kuwa wilaya ya Uvinza ina eneo lenye ukubwa wa hekta elfu 32 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa KASHUGULU ni miongoni ya mikakati ya kuzitumia hekta hizo.

Read 1266 times