Wednesday, 25 March 2015 00:00

9 wafa ajali ya gari Tabora.

Gari lilopata ajari na kusababaisha vifo,Tabora.(PICHA/LM)

Na Mwandishi wetu

WATU Sita wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne kugongana katika kijiji cha Undomo wilayani Nzega mkoa wa Tabora barabara ya Singida-Shinyanga.

Ajali hiyo iliyotokea machi 23, usiku imehusisha Basi la Kampuni ya Super Shem yenye nambari za usajili T 874 CWE, Lori aina ya CENTER T 831 DDK na magari madogo mawili likiwemo gari la Halmashauri ya wilaya ya Nzega yenye namba za usajiri SM 4905.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Nzega Dakta Erick Mbuguje amethibitisha vifo hivyo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea kutibiwa.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Rsalia Magoti amewataja waliokufa kuwa ni Dereva wa Gari la Halmashauri Charles Sanga, Mhasibu Emmanuel Katemi, Bwana afya Peter Steven na Robert Kisabho aliyekuwa katika mafunzo ya vitendo katika Halmashauri hiyo, na Matukuta Malikita alikuwa ni mfanyakazi wa zimamoto, huku marehemu Yasinta Alex akitajwa kama abiria aliyepewa msaada katika gari hiyo.

 Chanzo:TBC

Read 3304 times