Wednesday, 14 January 2015 03:00

ACT kwa chafuka,timua timua yaanza,Mwenyekiti Limbu,avuliwa madaraka

Chama cha ACT-Tanzania kimewavua uongozi viongozi wake,mwenyekiti wa  muda Kadawi Limbu,naibu katibu mkuuu (bara)Leopold Mahona na mwenyekit wa ngome ya vijana Graiyson Nyakarungu.

Katibu mkuu ACT, Samson Mwigamba  alisema maazimio ya mkutano huo yaliwachagua Shaaban Mambo kuwa mwenyekiti wa muda, Mohamed Masaga, Naibu katibu mkuu na Hassan Abdalah Omary kuwa mwenyekiti mpya wa vijana.

Aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa chama cha ACT Kadawi Limbu aliyesimamishwa uongozi wake ndani ya cha hicho.

Kwa upande wake, Limbu alisema siyo sahihi kwani mkutano huo hauna mamlaka ya kumwondoa kwenye nafasi yake bali ni kamati kuu tu ndiyo ina uwezo huo.

Maamuzi ahayo yamekuja baada ya kufikia maamuzi ya halimashauri kuu ya chama hicho,iliyokutana kijadili ajenda za nidhamu ya mwenyekiti wa,kupokea na kupitisha mwongozo na kanuni za uchaguzi pamoja na kushiriki uchaguzi huo mkuu ujao.

 

 

 

 

Read 2113 times