Saturday, 14 March 2015 00:00

Afisa elimu atakiwa kuchunguza matokeo mabovu kidato cha nne.

Mkuu wa mkoa wa Tanga,Said Magalula,(PICHA/LM)

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Said Magalula amemuagiza afisa elimu wa mkoani humo Ramadhani Chomola kufanya uchunguzi wa matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2014 katika mkoa huo. Magalula ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka. huu. Mkoa wa Tanga ndiyo mkoa uliofanya vibaya katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2014,mara baada ya matokeo kutoka katika shule kumi za mwisho kwa ufaulu nchini ,tano zinatoka mkoa wa Tanga.

mkuu wa mkoa wa huo Said Magalula akiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa RCC na kutoa agizo kwa afisa elimu mkoa Ramadhani Chomola.Katika hatua nyingine  Magalula amezungumzia uharibifu wa vyanzo vya maji unaofanyika katika misitu ya Amani wilayani Muheza na kutaja takwimu za upatikanaji wa maji mkoani hapa ambapo amesema hali ya upatikanaji wa maji kwa vijijini ni asilimia 54.6,wakati mjini ni asilimia 94.5,hivyo kuwataka watendaji kushiriki kikamilifu ili kumaliza tatizo hilo.

Shule zilizofanya vibaya ni Mashindeni na Magoma kutoka Korogwe vijijini,Mnazi na Manolo kutoka wilaya ya Lushoto na Kwalugulu ilioko wilaya ya Handeni.

Read 2828 times