Tuesday, 17 February 2015 00:00

Albino Atekwa Geita,wawili wanusurika.

Kijana mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi albino ametekwa na watu wasio julikana na kutoweka nae wilayani Chato mkoani Geita

Kijana huyo anayejulikana kwa jina Yohana Bahati,motto wa Bahati Misalaba mwenyeji wa Geita,alitekwa na watu wasiojulikana akiwa na baba yake baada ya kuvamiwa  na watu waliokuwa na silaha za jadi na kuwaweka chini ya ulizi na kumchukua Yohana na kutokomea naye kusikojulikana jana usiku..

Taarifa zinasema kuwa watu waliokuwa na silaha waliwaweka chini ulinzi wazazi hao,ambao walikua wameongozana na mwanae,ambapo alilazimika kujeruhiwa vibaya kupigani mwanae asichukuliwe purukushani ambayo haikuwa na mafanikio kwa mzazi huyo.

Aidha watoto wengine  wa  familia ya Bahati Msalaba ambao ni Tabu Bahati mwenye umri wa miaka miwili na Shida Bahati mwenye miaka kumi na mmoja ni walemavu wa ngozi walinusurika kutekwa na watu hao,ambapo wakati tukio linatokea nyumbani, wao walikuwa wameenda kucheza kwa majirani

 

Kwa mujibu wa taarifa za mwandishi kutoka eneo hilo Renatus Masuguliko, polisi wamefika eneo la tukio na kuanza msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho.

Matukio ya kuwaua na kuchukua viungo vya albino yaliyasambaa katika mikoa ya kanda ya Ziwa kutokana na imani za kishirikina kuwa viungo vya watu hao vingeweza kuwapatia utajiri na mafanikio mengine katika maisha yao, jambo ambalo ni upuuzi mtupu.

Baada ya tukio hilo polisi walifika  katika eneo hili na kuanza msako mkali kuwatafuta wale wote waliotenda unyama huo ambo umekuwa ukizidi kushamiri kwa imani za kishirikina.

Read 1567 times