Monday, 09 March 2015 00:00

Albino mwingine akatwa Giganja cha mkono Rukwa.

Kukiwa bado hali si shwari katika mikoa ya kanda uya ziwa kwa watu wenye ulmavu wa ngozi licha ya serikali kulivalia njuga swala hilo,mtoto mwingine aliyejulikana kwa jina  Braka Cosmas amekatwa giganja cha mkono.

Tukio hilo  limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi,ambapo wakati motto huyo alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri huku Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.

Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino, Na muda mfupi baada ya Rais Tanzania Jakaya Kikwete kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.

Read 2604 times