Friday, 20 March 2015 00:00

Asasi 300 kutoa elimu ya katiba baada ya kura ya Maoni katiba inayopendekezwa.

Jaji mstaafu,Mwenyekiti wa NEC,Damian Lubuva.(PICHA.LM)

Na Emmanuel Ndaki

Ikiwa zimebaki siku 42 kuingia katika hatua adimu ya kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa hapo Aprili 30 mwaka huu,hatua ambayo itatupeleka katika uchaguzi mkuu hapo oktoba,kumejitokeza asasi zaidi ya 300 ambazo zimeidhinishwa na tume ya taifa ya uchaguzi ambazo zinatarajiwa kutoa elimu ya Katiba siku chache mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuipigia kura katiba inayopendekezwa.

Jaji mtaafu na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Damian Lubuva amesemahayo katika mahojiano na kituo kimoja cha habari mkoani Njombe wakati wa zoezi uzinduzi awamu yapoli ya uandikishwaji kweny daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya BVR.

Kuhusu kura ya maoni,jaji Lubuva amesema kuwa kwasasa tume yake inaangali uwezekano wa kukamilisha mchakato wa kuwaandikisha wananchi woote wenye sifa za kujiandikisha ,na kama itatokea muda wa kupiga kura ukawa tofauti,basi wananchi watatangaziwa tarehe mpya ya kupiga kura. 

Read 1692 times