Tuesday, 24 March 2015 00:00

Ask Indus yafungua ofisi Tanzania.

Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal pamoja na wageni wengine wakishuhudia.

Na Mwandishi Wetu,

KAMPUNI ya ‘Ask Indus Global’ imezinduwa huduma zake nchini Tanzania kwa kufungua ofisi itakayowaunganisha wananchi kupata huduma mbalimbali kutoka India wakiwa Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi wa ofisi nchini Tanzania,Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Ask Indus Limited Abhilash Puljal amesema shabaha kubwa ya kufungua ofisi Dar es salaam ni kuweka daraja kwa wananchi watakakuwa na uhitaji wa huduma katika maswala ya Elimu,Afya na Biashara nchini India.Meneja wa Ask Indus Tanzania, A. Prakash (kulia aliyesimama) akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kabla ya kumalizika kwa hafla hiyo.

Aidha amesema kuwa ufunguzi wa ofisi hii itakuwa kiungo kwa wafanyabiashara wadogowadogo nchini Tanzania ambao wanaahagiza bidhaa kutoka India,ambapo wataweza kuunganishwa na kupata mahitaji ya kwa ghalama nafuu na bila usumbufu,ambapo mbali na huduma hizo,bado ofisi hiyo itaratibu huduma za kimatibabu za awali wakiwa Tanzania kwa kuwaunganisha na madaktari waliokuwapo India.

Mbali na Tanzania pia ofisi hiyo ipo nchini Kenya ambayo itakuwa kiungo kikubwa cha kuratibi huduma kutoka nchini India,ambapo kwa upande wake balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw amesema kuwa ofisi hii ni fursa pekee kwa wananchi waTanzania kupata ukaribu wa huduma wazitakazo wakiwa hapahapa Tanzania.

Read 1530 times