Thursday, 26 March 2015 00:00

Askari wawili mbaroni kwa tuhuma za mauaji.

PICHA kutoka Maktaba.

Na Mwandishi wetu

Askari wa wili wa jeshi la polisi wilayani Misungwi wa kituo kikuu wanashikiliwa kwa tuhuma za kuusika na mauji ya meneja wa nyumba ya kulala wageni,kilichotokea machi 24 mwaka huu, Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mwajuma Nyiruka amethibitisha kukamatwa kwa askari hao.

Wanaoshikiliwa na Polisi ni PC Kelvin na PC Omary wa kituo kidogo cha wilaya kwa kuhusika na kifo cha Magada Edson meneja wa nyumba ya kulala ya Rachel,ambao askari hao wanadaiwa kumpiga na kumjeruhi marehemu baada ya kwenda kutoa taarifa ya tukio la ubakaji lilotokea kwenye nyumba hiyo na kujikuta akipokea kipigo na kujeruhiwa  kiasi cha kukimbizwa Hospitali ya wilaya ya Misungwi kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Sokotoure na baadaye kufariki dunia.

Read 2072 times