Tuesday, 13 January 2015 03:00

Baadhi ya watumishi wa wizara ya ujenzi wamkacha Magufuli

Watendaji wa wizara ya ujenzi wamkimbia Wairi Pombe Magufuli kwa kile kinachodaiwa ni ukiritimba  na ubwana katika idara ya usalama barabarani.

Waziri ya Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli.

Uchunguzi  umebaini kuwa  idara hiyo inayoongozwa na Julius Chambo  Kaimu Mkurugenzi imekimbiwa na vigogo watatu ambao ni Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson Nkundineza ambao wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja.

Uchunguzi  umebaini kuwa  idara hiyo inayoongozwa na Julius Chambo  Kaimu Mkurugenzi imekimbiwa na vigogo watatu, Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson Nkundineza ambao wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja, .tangu Chambo ahamishiwe katika idara hiyo akitokea kituo cha mizani Himo mkoani Kilimanjaro, utendaji wa kazi umekuwa ukisuasua  kwa madai wanaongozwa kidikteta.

 

 

 

 

 

Read 1680 times