Thursday, 20 November 2014 03:00

Benjamin William Mkapa Hiv/Aids Foundation yafadhili Wanafunzi 888


Ufadhili Wa Mafunzo Kwa Wanafunzi 888 Watakaojiunga Na Mafunzo Ya Kozi Za Ngazi Ya Cheti (Certficate Level) Chini Ya Mfuko Wa “Global Fund” Round 9 Kupitia Taasisi Ya Benjamin William Mkapa Hiv/Aids Foundation
 
Taasisi ya Benjamin WIliam Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund – Round 9), inatekeleza mradi wa kuimarisha mifumo ya kutoa huduma za afya nchini. Moja ya Mikakati iliyowekwa ni kutoa ufadhili kwa wanafunzi mia nane themanini na nane (888) wanaojiunga na masomo ya ngazi ya Cheti katika vyuo vya afya vya Serikali, Binafsi na Mashirika ya Dini nchini.
 
Ufadhili huu utakuwa kama ifuatavyo
•    Ufadhili katika Vyuo vya Serikali utafuata mwongozo wa uchangiaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
•    Ufadhili wa Vyuo Binafsi na Mashirika ya Dini utakuwa kwa asilimia hamsini (50%) ya gharama za mafunzo iliyoainishwa kwenye barua ya kujiunga na masomo (joining instructions) 
 
Ufadhili huu utakuwa kwa miaka miwili kuanzia mwaka wa masomo 2014/15 hadi mwaka 2015/16 na utalipwa moja kwa moja katika akaunti ya Chuo alichochaguliwa Mwanafunzi. Aidha, ufadhili huu hautahusisha kulipa gharama zozote za ziada zitakazotokana na mwanafunzi kurudia mwaka au kuachishwa masomo kwa sababu zozote zile.
 
Ili kukamilisha taratibu za ufadhili, mwanafunzi atatakiwa kuridhia kwa maandishi kukubali ufadhili huu kwa kusaini hati ya makubaliano baina yake, Meneja wa Mradi (Taasisi ya Mkapa Foundation) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika, ili kuonyesha ridhaa ya kuajiriwa na Serikali mara baada ya kuhitimu masomo.
Kupata Orodha kamili ya waliochaguliwa katika ufadhili huu tafadhali bonyeza hapa
Kama inavyofahamika Baraza la Vyuo vya Ufundi la Taifa (NACTE) imekwishawapatia taarifa wanafunzi hivi sasa juu ya vyuo walivyochaguliwa kujiunga na masomo yao katika mwaka wa masomo 2014/15 na hivyo kila mwanafunzi atatakiwa kuripoti mara moja kwa Mkuu wa Chuo husika ili kukamilisha uwekaji sahihi wa mikataba akiwa Chuoni. 


Taasisi ya BMAF inawataarifu kila mwanafunzi aliyepata ufadhili huu akadurufu barua za kuelezea ufadhili huu kwa maelezo ya kina zaidi ili aweze kuzitumia wakati wa kuripoti kwa Mkuu wa Chuo husika,kupata barua ya vyuo vya serikali bonyeza hapa na kupata barua ya vyuo binafsi bonyeza hapa
 
Pale yanapohitajika maelezo ya ziada juu ya ufadhili huu, tafadhali wasiliana na Christine Malembeka kwa simu 0784 640375 au kupitia barua pepe ya: studentgrants@mkapahivfoundation.org  au na Maafisa katika ofisi za kanda husika za Taasisi ya BMAF kama ifuatvyo ;
 

 

 

Na

Mikoa

Mhusika

Simu

Barua pepe

  1. 1.

Mwanza, Kigoma, Shinyanga, Geita, Mara, Simiyu, Kigoma, Tabora na Kagera

 

Bw. Remmy Moshi

0784 481750

0717 263445

rmoshi@mkapahivfoundation.org

  1. 2.

Rukwa, Katavi,Iringa, Mbeya, Ruvuma, SIngida   na Njombe

Atuganile Jonas

0769424442

0784424442

 

ajonas@mkapahivfoundation.org

  1. 3.

Mtwara na Lindi

Joan Mungereza

0713270157

0787616101

jmungereza@mkapahivfoundation.org

  1. 4.

Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara

Restituta Masao

0754762934

0715762934

0782053269

 

rmasao@mkapahivfoundation.org

  1. 5.

Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma

Christine Malembeka

0784640375

0655640375

cmalembeka@mkapahivfoundation.org

 

 

Read 5678 times