Wednesday, 21 January 2015 00:00

Benki ya Dunia yatoa makadirio kuhusu hasara ya Ebola Afrika

Kulingana na uchambuzi wa Benki ya Dunia athari za kiuchumi za janga la Ebola zitaendelea kulemaza uchumi wa Guinea, Liberia, na Sierra Leone licha ya kupungua kwa kiasi kikubwa kwa viwango vya maambukizi katika nchi hizo tatu.

Rais wa benki ya dunia, JIM YONG KIM( PICHA/LM

Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, nchi hizo tatu zitapoteza angalau dola bilioni 1.6 ya ukuaji wa kiuchumi mwaka 2015 kutokana na Ebola.Madaktari wakujitolea wanaoendesha harakati za kupambana na ugonjwa wa Ebola Afrka Magharibi.PICHA/LM

Lakini ripoti hiyo mpya iliyotolewa usiku wa kuamkia Mkutano wa Dunia Kuhusu Uchumi 2015, Davos ina habari nzuri kwamba uwezekano wa kuenea kwa gharama za kiuchumi nje ya nchi tatu zilizoathiriwa pakubwa ni ya chini sana kuliko ilivyokadiriwa awali, chachu ikiwa ni juhudi za kina za kitaifa na kimataifa dhidi ya janga hilo katika kipindi cha miezi kadhaa.

Makadirio ya kiuchumi ya Benki ya Dunia ya  Oktoba 8, 2014 yaligundua kuwa Afrika Maghrabi ingepoteza dola bilioni 25 kama hasara za kiuchumi katika mwaka 2015, lakini ripoti ya sasa ya makadirio ya jumla ya hasara ya chini zaidi kwa mataifa ya Afrika yaliyoko chini ya jangwa la Sahara ni kama  dola milioni  500, huku kiwango cha juu kikiwa kama dola bilioni 6.2.

 

 

Read 1163 times