Thursday, 12 March 2015 00:00

Boda boda wachangia ujenzi wa shule Kibaha.

Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka.(PICHA/LM)

Kutoa ni moyo ndiyo kauli ambayo inaweza kutumika kwa watu wenye kipato cha chini,jambo ambalo linaweza kuchangia maendeleo kwa vizazi vijavyo hasa katika huduma za msingi za kijamii,ikiwamo Hospitali,Shule,na Madawa.

 Tatizo lililokuwa likiikabiri shule ya msnigi ya mailimoja kwa miaka minne tangu kuanguka kwa madarasa yake sasa inaonekana kutafutiwa fumbuzi baada ya wafanyabiashara waendesha pikipiki(Boda boda) katika mji wa kibaha,mkoani Pwani kuchangia fedha za ukarabati wa madarasa  na vyoo yaliyoanguka miezi minne iliyopita.

 Akikabidhi  mifuko ya Saruji mbele ya jumuiya ya wazazi,wanafunzi wa shule za msingi pamoja wakuu wa mamlaka ya mji wa kibaha, kwaniaba ya vijana hao,mbunge wa Kibaha Slivestry Koka amesema kuwa vijana hao wameamua kujitolea mifuko hiyo ya saruji kama mchango wao katika kuunga mkono juhudi za serikalai za kuboresha sekta ya elimu.

Mapema akizungumza kwa niaba ya walimu wakuu wa shule za msingi, mwalimu mkuu wa shule ya msingi mail moja Joyce Kilanjo amesema msaada uliotolewa utasaidia kukarabati na kujenga vyoo pamoja na madarasa yalioharibika katika shule hizo ambazo kwa sasa zinakabiliwa na tatizo kubwa la ubovu na uhaba wa vyoo.

 

Read 1744 times