Wednesday, 11 March 2015 00:00

Breaking News...Basi la ua vibaya Mafinga,Iringa leo.

Taarifa za awali kumetokea ajali katika eneo la Changarawe,wilayani Mafinga mkoani Iringa leo,ambazo zinaeleza kuwa watu wasio na idadi kamili wameripotiwa kufariki kufuati basi walilokuwa wakisafiria la Majinja likitokea Mbeya lenye namba za usajili T438 CDI,kuangukiwa na kontena.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajari hiyo wamesema kuwa inasadikiwa chanzo cha ajari hiyo ni ubovu wa barabara kutokana na eneo hilo kuwa na shimo kubwa ambalo lilisababisha basi hilo kutumbukia mara baada ya kugogwa na roli na kupindukiwa na kontena ambalo halijulikani lilikuwa limebeba nini.

Lakini kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani IRINGA Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,wakati jeshi la polisi likendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajari na idadi ya watu waliokufa.

Read 2390 times