Monday, 09 March 2015 00:00

Breaking News….Migodi 15 yateketea kwa Moto leo.

Migodi zaidi ya 15 ya machimbo ya madini ya Tanzanite kitalu B Mererani,wilayani  Simanjiro mkoani arusha ,imeteketea kwa moto uliosababishwa na mafundi wa  Tanesco ambao walikuwa wakitengeneza mita iliyokuwa jirani na machimbo hayo.

Gharama ya vitu na mali zilizoteketea inakadiliwa kiasi cha Bilioni 4 fedha za kitanzania,ambapo kuteketea kwa machimbo hayo yamesababisha kiasi ya wachimbaji wadogo zaidi ya 1000 kukosa makazi,tukio hilo limepelekea watu wa madini kufika na kuiomba serikali kufanya tahmini na kulipa fidia kwa wakati ili watu waendelee na kazi zao.

Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea www.livemedia.co.tz

Read 1714 times