Tuesday, 10 February 2015 00:00

BRN kuondoa uhaba wa watumishi wa Afya:Naibu waziri wa Afya Dk Kabwe.

 

Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk Kabwe Stephen Kabwe.

Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii DK Kabwe Steven Kabwe amesema chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa BRN,serikali imepania  kupunguza  uhaba wa watumishi katika sekta ya afya ili kuboresha huduma za afya kwa vifo vya mama na motto hapa nchini.

Akizungumza mjini Arusha kwenye mkutano wa kimataifa  wa sekta ya afya barani Afrika amesema mpaka sasa serikali imajiri watumishi 9000 kwenye mikao mitano kati ya tisa  hapa nchini yenye uhaba mkubwa wa watumishi.

Read 1713 times