Monday, 09 March 2015 00:00

China Kusaidia Tanzania.

Baada ya Tanzania na China kutiliana saini mikataba mbalimbali ya kimaendeleo,China imesema kuwa itaongeza jitihada zaidi katia diplomasia  na nchi za Afrika  katika sekta muhimu ikiwamo Viwanda,Afya, na kuimarisha usalama na amani.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje wa china Wang Yi katika mkutano na waandishi wa habari wakiwa wakijibu maswali juu ya etendaji wa kazi za wizara katika kipindi ambacho Bunge la china  (NPC)  linaendelea na vikao vyake.

Waziri Wang Yi amesema kuwa China itaendelea na ushirikiano hususani katika Nyanja ya  nguvu za maendelo ya Viwanda.ushirikiano katika sekta ya Afya kwa kuwajengea uwezo wananachi kuweza kupamabana na magonjwa,kusaidia usalama na kudumisha amani,kupambana na vikundi vya kigaidi na vita vya ndani kwa ndani.
Wakati wa ziara ya rais wa China  XI Jiping  nchini Tanzania March 2013, serikali ya China na Tanzania zitiliana saini ya ushirikiano katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo, mawasiliano, nishati na miundombinu,ilihali katika kupambana na magonjwa China tayarin imepeleka watumishi wa afya 100 katika nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola.
Mwezi uliopita China iliteua mwakilishi wa kudumu katika umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuimarisha mahusiano na bara la Afrika.
Mawaziri mbalimbali kutoka barani Afrika na wale wa China wanatarajia kukutana kwenye  Mkutano wa sita kuhusu ushirikiano wa mataifa ya Afrika na China (FOCAC) unatarajia kufanyika baadae mwaka huu nchini Afrika ya Kusini.

Read 1883 times