Thursday, 12 March 2015 00:00

CUF wagomea sheria ya kura ya maoni kujadiliwa,Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Kificho

Wawakilishi wa chama cha wananchi CUF visiwani Zanzibara wamegomea kujadilia sheria ya kura ya maoni namba 11 ya mwaka 2013 ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,jambo ambalo limesababisha Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho kulazimika kuharisha kikao hiko kilichokuwa kinafayika Kisiwani Unguja.

Mgomo wa wawakilishi wa CUF,na kuharishwa kwa kikao hiko kinafuatia baada ya mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Said Hassan Said kuwasilisha sheria hiyo ya kura ya maoni ya mwak 2013.

Kwa upande wake spika wa baraza la wawakilishi  Kificho amesema kuwa uwasilishwaji wa  mswada wa sheria hiyo ya maoni umezingatia kanuni za kisheria,hukua akisistiza kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa itafanyika kwa mujibu wa sheria.

Read 1689 times