Thursday, 26 March 2015 00:00

Dereva akutwa na magunia 11 ya Dawa za kulevya

Gari kampuni ya Wengert Windrose Safari,likiwa na magunia ya Bangi.(PICHA/LM)

Na mwandishi wetu

Juzi baada ya Serikali kupitisha mswada wa sheria wa kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya mjini Dodoma katika kikao cha 19 cha Bunge la jamhuri la muungano bado sakata la uingizwaji wa madawa ya kulevya nchini imekua changamoto baada ya jeshi la polisi mkoani Arusha kukamata gari likiwa linasafirisha madawa ya kulevya aina ya Bangi.

Gari hilo kampuni ya Wengert Windrose Safari ambalo linafanya kazi uwindaji wa kitalii limekamatwa likiwa linasafirisha Bangi kinyume na sheria za nchi.

Kwa mujibu wa kamnda wa polisi mkoani Arusha Lebaratus Sabas amesema kuwa gari hilo lenye namba za usajiri T695 ARR likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina la Frank Faustine limekutwa na magunia 11 wilayani Longido majira ya saa tano usiku yakisafirishwa  kwenda nchi ya jirani.

Hata hivyo kwa mujibu wa meneja wa maendeleo ya jamii ya kampuni hiyo ya Wengert Safari Bi Aurelia Mtuy amemkana derva wa gari hilo kwa kusema kuwa madawa yaliokamatwa si mali ya kampuni bali ni mali ya dereva mwenyewe,huku akilishukuru jeshi la polisi kwa kuweka wazi utovu wa nidhamu na maovu ya kwa baadhi  ya madereva wanaokihuka sheria na maadili ya kazi zao.

Read 2451 times