Saturday, 14 March 2015 00:00

'Migogoro ya Ardhi tatizo sugu,K/nondoni' -DC Makonda

Mkuu wa wilaya K/nondoni,PAUL MAKONDA,(PICHA/LM)

Mtu mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni mchungaji wa kanisa la Pentekoste kata ya wao aliyejulikana kwa jina Peter Mibilale anatuhumiwa kwa kosa la utapeli wa ardhi,ambo mkuu wa wilaya ya Kinondoni ameagiza hatua zaidi zichukuliew juu yake.

Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua za kisheria Peter Mibilale kwa kutuhumia kufanya utapeli wa ardhi kwa kutumia cheo cha mwenyekiti wa kijiji. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makonda amesema tangua aingie kazini , ofisi yake imeanza kushughulikia tatizo sugu la migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kinondoni na kuziagiza mamlaka husika kuchunguza tuhuma za mtu huyo ili sheria ichukue mkondo wake.

 “Imenibidi nicheke kwa sababu naangalia ni jinsi gani ya kutatua migogoro ya ardhi katika eneo hili, bado tena kiongozi wa kiroho na ambaye nimeambiwa ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa,  badala ya kushirikiana na wananchi, anaongeza kasi ya migogoro…achunguzwe na achukuliwe hatua,” alisema.

Aidha kwa mujibu wa Afisa ardhi manispaa ya Kinondoni Jeriman Masinga amesema kuuza ardhi isiyokuwa yako ni kinyume na sheria na pia ni kosa la jinai

“Mwenyekiti wa kiji hana mamalaka yoyote ya kisheria kuuza ardhi,mwenye mamlaka ya kuusika na maswala ya ardhi ni halmashauri za manispaa kwa kushirikiana ja mipango miji na upimaji wa ardhi”.

Badala yake, alishangaa  Februari 21, mwaka huu alipewa barua na serikali ya mtaa ikimtaarifu kujibu shitaka la kuvuka mipaka na kuingia eneo jingine lililotengwa na wananchi kwa shughuli za kijamii na kusitishwa kutolifuatilia tena eneo lake.

Hata hivyo, alisema kwa kutumia wadhifa wake, mwenyekiti huyo alichukua eneo hilo kwa nguvu na kumuuzia mwananchi mwingine kwa Shilingi milioni nne. 

Alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo kwa njia ya simu jana, mwenyekiti huyo alikata simu na baada ya mwandishi kujaribu kwa mara nyingine simu hiyo haikupatikana.

 

 

Read 1635 times