TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka za
Ajira mbalimbali anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya
kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 15/03/2018 na 17/03/2018 kama
ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu ambapo usaili
utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na Kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha Uraia
au Hati ya kusafiria;
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
v. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement
of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi
results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA
NA USAILI;
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE);
ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi
nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yaTangazo husika.
x. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na Vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi.

 

Kusoma majina hayo bofya hapo chini

Published in NAFASI ZA KAZI