Halmashauri ya Wilaya ya Geita

Kuitwa Kwenye Usaili (Nafasi za Aajira ya Mkataba Kada ya Afya)
Advrert Rf: No. GDC/AF/MAT/V.1/6 OF 9/3/2018

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, anawatangazia na kuwakaribisha waombaji wote wenye sifa waliofanikiwa kuchaguliwa na kuorodhoshwa kwa usaili kuhudhuria zoezi la usaili kuamzia jumatano tarehe 11 hadi Ijumaa 13 April 2018 ili watakao faulu usaili waweze kujaza jumla ya nafasi 34 za ajira kwa kada ya Afya chini ya ufadhili wa Mdau wa Maendeleo ya Afya AGPAHI

ili kuyasoma majina hayo bofya hapa chini

Published in NAFASI ZA KAZI

Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Geita

KUMB.NA GDC/AF/MAT/V.1/6

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo ya Afya, Shirika la AGPAHI, anawatangazia wananchi wote wenye sifa ya kuomba kujaza jumla ya nafasi 34 za kazi za kada ya Afya

1. AFISA TABIBU (CO) II TGSB B TZS 680,000/= NAFASI 11

SIFA ZA KUAJIRIWA
- awe amehudhuria na kufuzu mafunzo ya utabibu (clinical medicine) ngazi ya stashahada katika chuo kinachotambulika na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU
- kutambua na kutibu wagonjwa wa kawaida
- kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake
- kufanya upasuaji mdogo
- kushiriki kupanga na kutekeleza huduma za afya ya msingi
- kueleimisha jamii na kutoa ushauri nasaha kwa wagonjwa
- kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za afya na mfuko wa jamii
- kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma
- kuanda na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kituo
- kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

2. AFISA MUUGUZI MSAIDIZI (ANO) II TGHS B TZS 680, 000/= NAFASI 11

SIFA ZA KUAJIRIWA
- Awe amehudhuria na kufuzu mafunzo ya uuguzi na ukunga (Nursing and midwifery training) NGAZI ya diploma katika chuo kinachotambulika na Serikali na kusalijiwa na baraza la wauguzi na wakunga Tanzania

KAZI NA MAJUKUMU
- kutoa huduma za uuguzi na ukunga
- kukusanya takwimu muhimu za afya
- kuwaelekeza kazi watumishi, wauguzi walio chini yake
- kueleimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
- kutoa huduma za kinga, tiba, afya ya uzazi na mtot
- kutoa huduma za wagonjwa majumbani na kutoa ushauri nasaha katika matatizo kwa mtu binaffsi au familia husika
- kuelekeza kusimamia mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi
- kufanya kazi nyingine atakayo pangiwa na mkuu wake wa kazi

3. MUUGUZI (NURSE) II TGHS A TZS 432,000/= NAFASI 11

SIFA ZA KUAJIRIWA
- Awe amehudhuria na kufuzu mafunzo ya uuguzi na ukunga (Nursing and midwifery training) NGAZI ya diploma katika chuo kinachotambulika na Serikali na kusalijiwa na baraza la wauguzi na wakunga Tanzania

KAZI NA MAJUKUMU
- kufanya kazi za uuguzi na ukunga na kuhudumia wateja katika ktuo ulichopangiwa
- kusimamia na kuratibu kazi za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi
- kutoa huduma za wagojwa na wateja wa majmbani
- kutoa huduma za afya kinga, afya tiba, afya ya uzazi na mtoto pamoja na huduma rafiki kwa vijana
- kuelimisha agonjwa kuhusu matatizo ya kiafya
- kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi
- kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kituo
- kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na kiongozi wake wa kazi zinazohusiana na elimu uzoefu na ujuzi wake

MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA) TGHS A TZS 432,000/= NAFASI 1

SIFA ZA KUAJIRIWA
- awe amefuzu mafunzo ya sayansi za maabara za afya (health laboratory sciences) ngazi ya cheti astashahada katka chuo kinachotambulika na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU
- kupima sampili zinazotolewa maabara
- kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa maabara za juu
- kuhifadhi na kufanya ukaguzi wa vitendanishi, vifaa, kemikali katika maabara
- kuweka kumbukumbu za fifaa na zana za kutolea huduma
- kufanya kazi nyingine atakazo pangiw na mkuu wake wa kazi

SIFA ZA UJUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

i/ awe raia wa Tanzania
ii/ awe na umri wa kuanzia miaka 18 na si zaidi ya miaka 45
iii/ awe na elimu ya sekondari na cheti cha taaluma cha kidato cha 6 au kidao cha 4
iv/ awe amehudhuria na kufuzu mafunzo stahili ya nafasi anayoomba
v/ awe na uwezo wa kutunza siri za wateja anaowahudumia
vi/ awe tayari kufanya kazi na kuishi mazingira yoyote hasa vijijini

ajira hizi ni za mkataba wa miezi 6 ambao unaweza kuhuishwa baada ya kipindi hiko kwisho ... waombaji watakaoitwa na kufaul zoezi la usaili watapangiwa kufanya kazi katika zahanati za NYARUGUSU, LWAMGASA, NYAMALIMBE, NKOME, KAKUBILA, NA KASOTA NA vituo vya afya vya KATORO, NZERA, KASHISHI, CHIKOBE, NA BUKOLI watumishi wanaofanya kazi kwa kujitolea watapea kipaumbele

JINSI YA KUOMBA
- andika barua ya maombi kwa mkono ukiambatanisha nakala za vyeti vyako vyote vya taaluma na ujuzi pia ambatanisha picha 2 za passport za hivi karibuni, barua zote za maombi zitumwe kwa kuwasilishwa mwenyewe mkononi ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Geita au kutumwa ka njia ya posta kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA,
"AJIRA ZA AFYA",
S.L.P 139
GEITA

AU
tuma kwa njia ya batua pepe [email protected]

mwisho wa kupokeo maombi ni tarehe 23/03/2018 saa 9:30 Alasiri

Published in NAFASI ZA KAZI
NAFASI ZA KAZI  OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA WENYE ULEMAVU - WAKALA WA USALAMA NA AFYA  MAHALI PA KAZI OSHA
 
Wakala wa usalama na Afya mahali pa kazi ni taasisi ya Serikali iliyoundwa kwa mujibu wa sheria ya wakala wa Serikali namba 30 ya mwaka 1997 ambayo majukumu yake yameidhinishwa katika sheria ya usalama na afya mahala pa kazi namba 5 ya mwaka 2003. Wakala pamoja na kazi nyingine una dhamana ya kusimamia usalama na afya za wafanyakazi waanapokuwa kazini
 
Ili kuhakikisha  kuwa wakala unatekeleza majukumu kama ilvyoidhinishwa katika sheria tajwa hapo juu mtendaji Mkuu anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zipatazo kumi na 6 za kada tofauti kama ifuatavyo
 
1. DEREVA II NAFASI 10
 
SIFA ZA MWOMBAJI
- awe na cheti cha kidato cha 4 
- awe na leseni ya daraja E au C1 ya uendeshaji wa magari
- awe na uzoefu wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali
- awe amehudhuria  mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari yanayotolewa na chuo cha mafunzo cha stadi VETA AU chuo kingine kinachotambulika na Serikali
- Waombaji wenye vyeti vya majaribio ya ufundi daraja la II watanza kufikiriwa
 
MAJUKUMU YA KAZI 
 
i/ kukaguaa gari kabla na baada  ya safari  ili kubaini hali ya usalama wa gar
ii/ kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbli kwenye safari za kikazi
iii/ kufanya mategenezo madogo madogo ya gari
iv/ kukusanya na kusambaz nyaraka mbali mbali
v/ kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
vi/ kufanya usafai wa gari
vii/ kufanya kazi nyingine kadri atakavyo pangia na msimamizi wake
 
MSHARA 
OSHA 3.1 kwa mwezi
 
MTUNZA KUMBU KUMBU MSAIDIZI  NAFASI 4
 
SIFA ZA MWOMBAJI
- awe na elimu ya kidato cha 4 au 6
- awe amehitimu mafunzo ya utunzaji kumbu kumbu katikka ngazi ya cheti  katka moja wap ya fani ya masijala  kutoka katika vyuo vinavyotambulika na serikali
 
MAJUKUMU NA KAZI 
i/   kutafuta kumbu kumbu, nyaraka na majalada yanayohitajiwa
ii/ kuthibiti upokeaji na uandikishaji a kumbu kumbu 
iii/ kuchambua , kuorodheshana kupanga kumbukumbu
iv/ kufungua majalada mapya yanayo hitajika
v/ kuweka kumbukumbu katika majalada, makabati reki katika masijala
vi/ kuthibitisha machapisho kwaajili ya kumbukumbu za ofisi ndani ya muda uliopngwa
vii/ kutoa elimu ya mar kwa mara kwa maafisa wanao kiuka utaratibu was uhifadhi wa kumbu kumbu
viii/ kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na msimamizi
 
MSHARA
OSHA 4.1 Kwa mwezi
 
MHASIBU MSAIDIZI NAFASI 4 
 
SIFA ZA MWOMBAJI
- awe na stashahada ya kawaida ya uhasibu  kutoka chuo/taasisi yoyote inayotambulika na serikali
- awe na cheti cha ufahulu wa mtihani mgumu wa uhasibu serikalini  (higher standard government accountacy examination) unaotelewa na chuo cha utumishi wa Umma
- awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja katika fani ya ushasibu
 
MAJUKUMU YA KAZI
i/ kupokea na kulpa fedha
ii/ kutunza dftari la fedha
iii/ kufanya suluhisho la hesabu za benki (bank reconciliation)
iv/ kukagua hati za malipo
v/kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
vi/ kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu
vii/ kufanya kazi nyingine atakayo pangiwea na msimamizi wake
 
MSHARA 
OSHA 4.1 kwa mwezi
 
MASHARTI KWA UJUMLA
- waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri wa miaka isiyozid 45
- waombaji waambatanishe cheti cha kuzaliwa
- waombaji waambatanishe maelezo binfsi yanayojitosheleza yenye anwani na namba za simu pamoja na  majina ya wadhamini wa 3
- maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakla za vyeti vya kidato cha 4 na 6 kwa wale walifika kidato cha 6
- waombaji waliosoma nje ya Tanzania  wakikishe vyeti vyao  vimehakikiwa na kudhibitiswha na mamlaka husika (TC/NECTA)
- WATAKAO WASLISHA TAARIFA ZA UONGO WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
- Maombi yatumwe kwa njia ya posta au kwa mkono  kufikishwa  ofisi za makao makuu zilizopo kinondoni bara bara ya mahakama
- mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 29/12/2017
- maombi yatakayao wasilishwa nje ya utaratibu hayatafanyiwa kazi
 
Jinsi ya kutuma maombi
 
Maombi yatumwe kwa
MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI,
S.L.P 519,
DAR ES SALAAM
 
SOURCE MWANANCHI DECEMBER 11 2017
 
Published in NAFASI ZA KAZI
 
 
 
MHE SELEMANI JAFO ASEMA TAARIFA ZA WATUMISHI 2058 WALIOAJIRIWA IMEKAMILIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) amesema jumla ya watumishi wa Sekta ya Afya wapatao 2058 wamekwisha pangiwa vituo vya kazi kuanzia leo 06/11/2017 na taarifa zote zinapatikana kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Taarifa ya watumishi 2058 imekamilika na itarushwa kwenye mtandao wa OR TAMISEMI leo tarehe 6/11/2017 jioni, hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wanatakiwa kujiandaa kuwapokea watumishi hao ikiwemo kuwapatia stahiki zao”

Amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waajiri kuhakikisha wanachukua taarifa za watumishi walioripoti na kuwaingiza kwenye Mfumo wa Mishahara na kuwapangia katika maeneo ambayo ya uhitaji mkubwa ili kuboresha huduma za afya nchini.
Pia ameekeza watumishi wanaopangiwa vituo, kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu tangazo hili kutolewa.

Aidha, Waajiri wote watoe taarifa juu ya kuripoti kwa watumishio haa wapya na vituo walivyopangiwa siku 14 baada ya kuripoti kwao.
Taarifa za Watumishi hao na Vituo vyao vya kazi, inapatikana katika Mtandao wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) wa www.tamisemi.go.tz
Published in MAKALA ZA AJIRA
Wednesday, 01 November 2017 06:35

TANGAZO LA KUITWA KAZINI WIZARA YA AFYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kumb. Na. CD. 162/355/01

30 Oktoba, 2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

OR TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika.

Aidha, mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti ya OR TAMISEMI www.tamisemi.go.tz. Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo, watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika.

Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya zitatangazwa mara baada ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa vyeti.

Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.

Limetolewa na:-
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
OR – TAMISEMI
30/10/2017

kusoma hayo majina bofya hapo chini

Published in KUITWA KWENYE USAILI

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA

Wizara ya Afya, Maendeleo, Jinsia Wazee na Watoto kupitia kibali cha Ofisi ya Raisi Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inatangaza nafasi za kazi 3,152 kwa wahitimu wa kada za afya chini ya Wizara ina jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya Utumishi Na. 1 wa mwaka 2009, kuhusu miundo ya utumishi  ya kada ya Wizara ya Afya nafasi zinanzotangazwa zifuatazo
1.    Ass. Lab.tech
2.    Technologist II
3.    Assistant nursing officer II
4.    Assistant clinical officer II
5.    Assistant Dental officer II
6.    Assistant medical officer II
7.    Assistant Nurse
8.    Assistant Pharmacist II
9.    Assistant Technologist
10.    Assistant EnviroNHealth Officer II
11.    Biomedical Eng. Techn II
12.    Clinical Assistant
13.    Clinical Officer
14.    Dental Surgeon II
15.    Dental Therapist II
16.    Environ. Health Ass. II
17.    Environ Health Officer II
18.    Health Lab Technologist II
19.    Health Lab Scientist Officer II
20.    Health recorder II
21.    Health Secretary II
22.    Laboratory technologist II
23.    Launderers
24.    Medical Attendant
25.    Medical consultant
26.    Medical Doctor II
27.    Medical specialist II
28.    Nurse
29.    Nursing Officer II
30.    Nutritionist II
31.    Occupational Therapist II
32.    Pharmacists Grade II
33.    Physiotherapist II

SIFA ZA MWOMBAJI
-    Awe ni raia wa Tanzania
-    Awe na umri usiozidi miaka 45
-    Asiwe mwajiriwa wa serikali au asiwe mwajiriwa wa hospital za mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na serikali
-    Asiwe ameshawahi kufanya kazi serikalini na kuacha

MAOMBI YAAMBATANISHWE NA
•    Nakala ya cheti cha taaaluma
•    Nakala ya cheti cha kidato cha nne/sita
•    Maelezo binafsi
•    Picha pssportsize 2 za hivi karibuni
•    Nakala ya cheti cha usajili au leseni ya kazi ya taaluma husika
•    Nakala ya cheti cha kuzaliwa

Nakala za vyeti vya taaluma  na vyeti vya kidatao cha nne vithibitishwe na hakimu au wakili
Wahitimu wote wa kada za afya zilizotajwa hapo juu mnaombwa kutuma maombi yenu kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo na si vinginevyo

KATIBU MKUU (AFYA),
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTOT,
CHUOKIKUU DODOMA,
KITIVO CHA SAYANSI NA MAENDELEO YA JAMII,
JENGO NO 11,
S.L.P 743,
DODOMA

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Agosti 2017
Tangazo hili linapataikana katika tovuti yetu ya www.moh.go.tz 

Published in NAFASI ZA KAZI

NAFASI ZA KAZI LODHIA STEEL INDUSTRIES LIMITED

Tuna karibisha maombi ya kazi kwa watu walio hitimu na wenye ujuzi na uzoefu katika nafasi zifuatazo

1.       WASIMAMIZI (NAFASI 3)  NA WAFANYAKAZI WENGI KWA

-          Kitengo cha neli(TUBEMILL)

-          Kitengo cha kupasua(SLITING LINE)

-          Kitengo cha kukata(CUT –TO LENGTH LINE)

2.       MAFUNDI UMEME WA NELI KUPASUA NA KUKATA

Wale wenye uzoefu wa miaka 3 watapewa umuhimu

3.       WAENDESHA KEREZO/MASHNE

-          Wale wenye ujuzi wa khali ya juu kuendesha mashine ndiyo wanapaswa kutuma maombi

4.       WASIMAMIZI

Wawe na shahada au stashahada ya ufundi mitambo(injinia)

5.       MAFUNDI UMEME(ELETRICIAN)

Wawe na shahada au stashahada ya injinia ya ktk uhandisi wa umeme na uzoefu wa uendeshajo wa virekebishi mitambo

6.       WATUNZA GHALA/NA WATUNZA GHALA WASAIDIZI

Ujuzi wa komputa na  ni lazima na pamoja uzoefu wa miaka 3 hadi 5 ya utunzaji wa ghala kwa mtunza ghala na ujuzi wan a uwezo wa kupanga mali kwa unadhifu kwa wasaidizi wa ghala

7.       MAKARANI WA KUAGIZA AU KUPOKEA BIDHAA

Uzoefu wa kazi hii inatakiwa watu wenye ujuzi watapewa  umuhimu. Awe na ujuzi wa kompyuta uwezo wa kuwakilisha taarifa katika iwsahili na kingereza

8.       MENEJA UTUMISHI/RASILIMARI WATU

Tunahitaji mwanasheria mwenye uzoefu na uhusiano na idara ya serikali inayohusika na sheria mtaartibu na anayeweza kutawala harira zake

9.       WAHASIBU

Wenye ujuzi wa kutayarisha taarifa za mahesabu wenye uelewa a miandao tofauti,uelewa wa sheria ya kodi, ya thamani (VAT) na sheria zinazohusu malipo. Mwombaji aweze kuzungumza Kiswahili na kingereza kwa ufasaha

10.   BWANA AFYA/USALAMA

Msimamizi na ujuzi mwenye ufahamu na maswala ya (health and safety) katika mazingira  hatarishi ya ufanyaji kazi kwa wafannyakazi na maeneoo yanayozungukia kiwanda kuzuia ajali na awe na ufahamu wa kutoa huduma ya kwanza

11.   KARANI WA MALIPO

Uzoefu wa miaka miwil katika nafasi hii aelewe shaeria zinazohusu malipo awe na ujuzi na kompyuta

12.   KARANI W MAPOKEZI

Mwombaji awe na mwonekano nadhifu, aongee kingereza na Kiswahili kwa ufasaha mjuzi wa kutumia cm za EPABX na mweny haiba nzuri

 

Maombi yatumwe yakiambatanishwa na CV  PAMOJA NA NAKALA ZA VYETI KA KUTUMIA EMAIL  [email protected] mwisho wa kupokea maombi tarehe 10 Oktoba 2018

Chanzo NIPASHE 6, OCTOBA 2016

Published in NAFASI ZA KAZI