MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI UTUMISHI TAREHE 14 APRIL 2018

Popular

Full Details

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/J/117 06 Aprili, 2018

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI), Chuo cha Taifa
cha Utalii (NCT) na Chuo Kikuu cha Ardhi, anatarajia kuendesha usaili na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

1. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 14/04/2018 kama ilivyoainishwa
kwenye tangazo hili, muda wa usaili umeainishwa kwa kila kada.

2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
Vitambulisho vinavyokubalika ni: Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi,
Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.

3. Wasailiwa wanatakiwa kufika na Vyeti vyao Halisi vya
kuanzia kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu,
Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

4. Wasailiwa watakaokosa Vyeti halisi na badala yake
kuwasilisha“Testimonials”, “ProvisionalResults”,“Statementof
results”, hati matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM
VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

5. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

6. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanya
usaili.

7. Kila Msailiwa anahitajika kufika na cheti halisi cha kuzaliwa

8. Kila Msailiwa afike na picha yake ‘passport size’

9. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe kuwa Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na
NECTA)

10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika
tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite
kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Kuona majina hayo bofya hapa https://www.ajirazetu.com/ajira/majina-ya-walioitwa-kwenye-usaili-utumishi-tarehe-14-april-2018

Ad details

Ad ID : 8325
Dar Dar es Salaam, Tanzania
6568 Views

Advertiser details

Ajira Zetu (1509)
Contact Advertiser Share

Phone number

Sorry, you need to register or login first.

MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI UTUMISHI TAREHE 14 APRIL 2018

Contact form

Sorry, you need to register or login first.

What's wrong with this ad?

Sorry, you need to register or login first.

Add to favorites

Sorry, you need to register or login first.